Du´aa unapohisi maumivu kwenye kiungo fulani

Swali: Vipi du´aa wakati mtu anapohisi ugonjwa:

“Kwa jina la Allaah.” mara tatu?

Jibu: Haya yamepokelewa na Muslim katika “as-Swahiyh” yake. Anapohisi ugonjwa aweke mkono wake pale maeneo anapohisi maumivu na aseme:

“Kwa jina la Allaah.” mara tatu.

أعوذ بعزة الله وقدرته من شر ما أجد وأحاذر

“Najilinda kwa nguvu na uwezo wa Allaah kutokamana na shari ya kile ninachohisi na kuogopa.”

Mara saba. Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake. Hii ni miongoni mwa du´aa zilizokusanya, nzuri na fupi.

Swali: Ataweka mkono wake pale mahali anapohisi maumivu?

Jibu: Ataweka mkono wake wa kulia, au wa kushoto, pale juu anapohisi maumivu.

Swali: Bila ya kutema cheche za mate?

Jibu: Haikupokelewa kuwa atafanya hivo.

Swali: Ataweka mkono wake mara moja au atakuwa mwenye kuunyanyua mara kwa mara?

Jibu: Hapana. Atauwacha juu yake. Hapana neno ikiwa atauweka na kuutoa, kuweka na kuutoa. Hata hivyo Hadiyth inasema kuwa ataweka mkono wake pale maeneo anapohisi maumivu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23144/ما-الدعاء-المشروع-عند-المرض
  • Imechapishwa: 11/11/2023