Yeye pekee ndiye anayesifiwa kwa kila hali

Swali: Je, kuna ubaya kusema:

“Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye hakuna mwingine  anayesifiwa kwa yanayochukiza isipokuwa Yeye tu?”

Jibu: Sitambui kuwa ina ubaya. Mtu anaweza kufikwa na jambo lenye kumchukiza, licha ya hivo akamuhimidi Allaah. Akifikwa na maradhi au msiba mwingine akamsifu na kusema:

الحمد لله على كل حال

“Himdi zote njema anastahiki Allaah kwa kila hali.”

إنا لله وإنا إليه راجعون

“Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea.”

Allaah (´Azza wa Jall) anasifiwa kwa kila hali, kwa sababu hahukumu hukumu isipokuwa ndani yake kuna kheri na manufaa.

Swali: Kwa hiyo maana yake ni sahihi?

Jibu: Ndio, maana yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23145/حكم-قول-الذي-لا-يحمد-على-مكروه-سواه
  • Imechapishwa: 11/11/2023