76. Ni nani ambaye Mtume Mtume alimwacha aswalishe wakati wa kuguua kwake?

Swali 76: Ni nani ambaye Mtume Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwacha aswalishe wakati wa kuguua kwake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwacha aswalishe swahiba yake pangoni na rafiki yake katika hali ya safari na ya ukazi, mtu wa kwanza ambaye alimsadikisha katika ujumbe wake na kujisalimisha kwa yale aliyokuja nayo, na khaliyfah wa kwanza juu ya ummah wake – Abu Bakr as-Swiddiyq. Allaah amuwie radhi na amridishe!

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 145
  • Imechapishwa: 11/11/2023