Swali: Anayetokwa na damu kidogo puani ni lazima aikate swalah yake?

Jibu: Hapana, kama ni ndogo ni yenye kusamehewa. Damu ndogo inayotoka puani, kwenye meno au kwenye macho ni yenye kusamehewa.

Swali: Vivyo hivyo kuhusu kutapika?

Jibu: Matapishi madogo yanasemehewa, lakini hayaitwi kuwa ni matapishi, kwa sababu matapishi ni lazima yakariri.

Swali: Matapishi ya mtoto mdogo wa kiume mchanga ni yenye kusamehewa pia?

Jibu: Ni kama mfano wa mkojo wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23254/حكم-الرعاف-والقيء-اليسيران-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 08/12/2023