Chukia shari kwa ndugu zako kama unavyoichukia kwa nafsi yako

Swali: Kinachopata kufahamika kwa Hadiyth hii[1] ni kwamba pia achukie kwa watu yale anayoyachukia juu ya nafsi yake?

Jibu: Ndio, achukie juu yao shari kama anavyochukia juu ya nafsi yake. Wanaweza kuwepo watu ambao wanachukia mambo ambayo hayatakiwi kuchukiwa. Anachotakiwa kuchukia ni shari. Baadhi ya watu wana mapungufu katika dini yao na hivyo ikawapelekea kuchukia Tawhiyd, imani na kadhalika. Anachotakiwa kuchukia ni shari. Aidha aichukie juu ya watu kama anavyoichukia juu ya nafsi yake. Muumini anachukia maasi yote na pia anayachukia juu ya ndugu zake.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule anayependa kuepushwa na Moto na kuingia Peponi kimfikie kifo chake hali ya kuwa anamwamini Allaah na siku ya Mwisho, na awajilie watu vile anavyopenda yeye kujiliwa.”” (Muslim (1844).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23439/هل-يجب-ان-يكره-المسلم-للناس-ما-يكره-لنفسه
  • Imechapishwa: 22/01/2024