Swali: Je, mtu afanyie kazi wasia ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amempa usingizini?

Jibu: Ni vyema ikiwa haupingani na Shari´ah. Ikiwa unaenda kinyume na Shari´ah ina maana ya kwamba sio Mtume na sio ndoto sahihi. Akiota usingizini kuwatendea wema wazazi, kuchunga swalah, kutoa zakaah na kupambana jihaad. Zote hizi ni ndoto njema na ni alama ya kheri.

Swali: Akimuona kwa mujibu wa sifa zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha akamuuliza swali na akamjibu?

Jibu: Ayapime kwa Qur-aan na Sunnah. Shari´ah imekamilika. Shari´ah ilikwisha katika uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Kama mfano wa baadhi ya Hadiyth wanamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu baadhi ya Hadiyth?

Jibu: Ndio. Muhimu ni kwamba akiota usingizini yanayopingana na Shari´ah asiyatendee kazi. Na ikiwa yanaafikiana na Shari´ah basi itambulike kuwa Shari´ah imekwishakamilika ndani ya uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23440/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%88%D8%B5%D8%A7%D9%87-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D8%A8%D8%B4%D9%8A%D8%A1-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%86%D8%A7%D9%85
  • Imechapishwa: 22/01/2024