223 – Rifaa´ah bin Raafiy´ amesimulia kwamba alikuwa ameketi na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alisema:

إنّها لا تتمُّ صلاةٌ لأحدٍ حتى يُسبغَ الوضوءَ كما أمرَ اللهُ، يَغسِلُ وجهَهُ ويَدَيهِ إلى المِرفقين، ويمسح برأسِه ورجليه إلى الكعبين

“Hakika haitimii swalah ya yeyote mpaka atimize wudhuu´ wake, kama alivyomwamrisha Allaah. Anatakiwa kuosha uso wake, mikono yake mpaka kwenye viwiko, kufuta kichwa chake na miguu yake mpaka kwenye fundo mbili za miguu.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/208)
  • Imechapishwa: 22/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy