Bora ni kunywa kwa kuketi chini, japo inafaa kusimama

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa bora ni kunywa maji ya zamzam kwa kusimama.

Jibu: Hapana, bora ni kwa kuketi chini. Lakini isipowezekana anywe kwa kusimama. Kanuni inasema kwamba wakati Maandiko yanataja makatazo na kukaja kitu chenye kuonyesha kinyume chake, basi makatazo hayo yanajulisha kuwa sio haramu.

Swali: Wanasema kuwa alikunywa zamzam kwa kusimama kwa sababu maeneo hapo palikuwa matope. Vinginevyo angekunywa kwa kuketi chini.

Jibu: Hapana, alikunywa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) vinywaji vingine mbali na zamzam. Kwa mfano wa Hadiyth ya Nazzaal bin Samurah[1] na Hadiyth ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). ´Aliy amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa kwa kusimama na alikunywa kwa kuketi chini.

[1] Abu Daawuud (3709).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23264/حكم-شرب-ماء-زمزم-قاىما
  • Imechapishwa: 16/12/2023