Bora ni anayeanza kusalimia

Swali: Wakati mwingine mtu anahisi uzito kuanza kusalimia kutokana na wingi wa wafanyakazi wa kikafiri.

Jibu: Wewe hukusikia nini alichosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa ni kitendo gani bora ambapo akajibu:

“Kulisha chakula na kumtolea salamu unayemjua na usimyemjua.”

Swali: Kuenea kwa dalili za salamu kunafahamisha ulazima wa kufanya hivo?

Jibu: Kuenea salamu ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Mtu akianza ndio bora zaidi. Ukianza kutolewa basi ni lazima uitikie. Muumini anakimbia mambo ya kheri ingawa kuanza kutoa sio lazima hata hivyo anatakiwa kuharakia kuanza. Ni kama mfano wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa:

“Ee Mtume wa Allaah! Ni Uislamu gani bora?” Akajibu: “Kulisha chakula na kumtolea salamu unayemjua na usimyemjua.”

Bora kwa mtu ni kuyakimbilia matendo mema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22624/ما-حكم-السلام-على-جمع-فيهم-غير-مسلمين
  • Imechapishwa: 09/07/2023