Kigezo cha kujifananisha na makafiri

Swali: Kuna kigezo kipi cha kujifananisha na makafiri?

Jibu: Mavazi yanavaliwa na wao tu. Haifai kwa waislamu wakayavaa. Lakini sio kujifananisha endapo wanashirikiana wote. Kwa mfano kupanda ndege, gari na kupanda treni sio kujifananisha. Kwa sababu wote wanashirikiana. Vivyo hivyo kutumia vifaru, mizinga na vyenginevyo vilivyovumbuliwa hii leo sio kujifananisha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22634/ما-الضابط-في-التشبه-بالكافرين
  • Imechapishwa: 09/07/2023