10. Swalah ndio ahadi kati ya muislamu na wao

44 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kati ya mja na ukafiri ni kuacha swalah.”

45 – ´Abiydah ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Sufyaan, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah mfano wake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1].

46 – Yahya bin Waadhwih ametuhadithia, kutoka kwa Husayn bin Waaqid: Nimemsikia Ibn Buraydah akisema: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni kuacha swalah. Yule mwenye kuiacha amekufuru.”[2]

47 – Shariyk ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaswim, kutoka kwa Zurr, kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:

“Yule ambaye haswali basi hana dini.”[3]

48 – Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia, kutoka kwa Hishaam ad-Dastawaaiy, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Abu Qilaabah, kutoka kwa Abul-Maliyh, kutoka kwa Buraydah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Yule mwenye kuacha ´Aswr, basi yameharibika matendo yake.”[4]

49 – ´Iysaa na Wakiy´ wametuhadithia, kutoka kwa al-Awzaa´iy, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Abu Qilaabah, kutoka kwa Abul-Muhaajir, kutoka kwa Buraydah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mfano wa Hadiyth iliyosimuliwa na Yaziyd, kutoka kwa Hishaam ad-Dastawaaiy[5].

50 – Hushaym ametuhadithia: ´Abbaad bin Maysarah al-Minqariy ametueleza, kutoka kwa Abu Qilaabah na al-Hasan ambao walikuwa wameketi chini ambapo Abu Qilaabah akasema: Abud-Dardaa’ amesema:

“Yule mwenye kuacha ´Aswr mpaka ikampita pasi na udhuru, basi yameporomoka matendo yake.”[6]

[1] Cheni hii na ile ya kabla yake ni kwa mujibu wa sharti za Muslim. al-Bukhaariy na Muslim wameipokea katika “as-Swahiyh” zao kupitia njia zingine kutoka kwa al-A´mash na huko Abuz-Zubayr ametamka wazi amehadithia kutoka kwa nani.

[2] Cheni ya wapokezi wake ni kwa mujibu wa sharti za Muslim. Imesahihishwa na at-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan, al-Haakim na adh-Dhahabiy.

[3] Hakimu Shariyk bin ´Abdillaah ni dhaifu kwa sababu ya kumbukumbu yake mbaya.

[4] al-Bukhaariy. Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.

[5] Ahmad (05/361) ameipokea kutoka kwa Wakiy´ peke yake. Ibn Maajah (964) na Ibn Hibbaan (256) wameipokea kupitia njia zingine kutoka kwa al-Awzaa´iy. Sahihi zaidi ni kile cha kwanza, kama ilivyo katika “Fath-ul-Baariy”.

[6] Kwenye upokezi wa al-Hasan kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi. Maneno ya Abud-Dardaa´ yamepokelewa pia kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa Ahmad (06/442). Lakini cheni hiyo imemtaja ´Abbaad bin Raashid al-Minqariy, tofauti na inavyosema hapa. Vivyo hivyo katika “al-Muswannaf” (02/186/12). Na ndio jambo lenye nguvu zaidi kwangu, kwa sababu sijamuona yeyote akimtaja Ibn Raashid kuwa ni al-Minqariy. Kwa hali yoyote, wote wawili ni wanyonge ingawa Ibn Raashid alikuwa msimuliaji imara zaidi kuliko Ibn Maysarah, kama ilivyo katika “Fath-ul-Baariy”. Kwa maana nyingine, hayafichikani yaliyomo katika maneno ya al-Mundhiriy aliposema:

“Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.” (at-Targhiyb wat-Tarhiyb)

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 25-27
  • Imechapishwa: 10/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy