Haifichiki kwmaba Shari´ah yenye hekima ambayo imewapa waja manufaa ya kidini, ya kilimwengu na ya kimwili imemkataza mfungaji kutoa damu na mfano wake kutoka mwili wake kwa ajili ya kumfanyia upole na kumlinda. Kwa sababu ikiwa mfungaji mchana wote amekatazwa kuingiza kitu tumboni katika virutubishi na vyakula, basi ikawa ni katika hekima mfungaji kukatazwa kutoa damu ambayo ndio inamfanya mwanadamu kuwa na nguvu na kuweza kuishi. Ndio maana katika Hadiyth kadhaa kumepokelewa makatazo kwa mfungaji kuumikwa. Kunatumiwa kama kipimo kila ambacho kina maana hiyo kukiwemo kuzuia na kuikata mishipa ili kutoa damu na kadhalika. Hiki anachotaka kufanya kwa lengo la kutibu maleria ni katika aina hiyo. Kwa hivyo mfungaji anatakiwa kukiepuka. Ingelikuwa ni vyema kama kusingelikuwa jengine zaidi ya kuzuia njia ili watu wasichukulie wepesi jambo la swawm. Hilo khaswa kwa kuzingatia kwamba watu hawana udharurah wa kufanya hayo yaliyotajwa katika mchana wa swawm, kwa sababu wako na usiku na wako na miezi kumi na moja mingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/192-193)
  • Imechapishwa: 14/03/2024