Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa Kaamil Mahmuud Habiyb – Allaah amlinde.

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Tumefikiwa na maswali yako matatu kwetu ambapo mawili katika hayo hayahusu kamati ya kutoa fatwa, kwa sababu ni magomvi ambayo yanatakiwa kupelekwa mahakamani. Swali la tatu linahusu mwanaume ambaye amemwingilia mke wake mchana wa Ramadhaan ilihali amefunga na akafanya naye mambo ya romantiki pasi na kufanya naye tendo la ndoa. Baada ya hapo akatokwa na manii kikamilifu. Anauliza yanayopelekea kwake juu ya kitendo hicho?

Napenda kukufahamisha kuwa funga yake ya siku hiyo imeharibika na analazimika kuilipa. Hahitaji kutoa kafara kwa sababu utoaji wa kafara ni jambo linahusu kufanya jimaa tu.

Muftiy wa Saudi Arabia

03/01/1385

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/191)
  • Imechapishwa: 14/03/2024