Bora kulipa swalah iliyokupita nyumbani au msikitini?

Swali: Kuna mtu ana mazowea mkusanyiko unapomaliza kuswali anasimama, akitawadha na kuswali peke yake msikitini kwa hoja kwamba kulipa swalah ya faradhi msikitini ni bora kuliko kuilipa nyumbani. Je, hilo lina dalili?

Ibn Baaz: Amekosa swalah ya mkusanyiko?

Mwanafunzi: Amekosa ile swalah ya kwanza ya mkusanyiko.

Swali: Udhahiri ni kwamba atailipa nyumbani. Hapana haja ya kwenda msikitini. Inatosha kuilipa nyumbani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23688/هل-قضاء-الفرض-بالمسجد-افضل-من-البيت
  • Imechapishwa: 04/04/2024