Wakati inapotakiwa na isipotakiwa kuadhiniwa

Swali: Mtu ambaye amelala na kukosa swalah aadhini kwa ajili yake?

Jibu: Msingi ni kuadhini hata kama wakati wa adhaana umeshatoka. Lakini ikiwa ni ndani ya wakati watu wameshaadhini na inatosha. Yeye atakimu tu. Lakini akiamka baada ya jua kuchomoza Sunnah ni yeye kuadhini na kukimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/هل-يوذن-للصلاة-الفاىتة
  • Imechapishwa: 04/04/2024