Bora mwanamke aswali nyumbani au Makkah na Madiynah?

Swali: Kipi bora kwa mwanamke anapokuwa Makkah na familia yake; aswali nyumbani au aswali katika msikiti Mtakatifu?

Jibu: Haijalishi kitu Makkah wala Madiynah. Bora kwake ni yeye kuswali nyumbani. Isipokuwa ikiwa kama kuna haja kwa mfano kusikiliza mawaidha, ukumbusho na mihadhara. Sababu nyingine inaweza kuwa anahisi uvivu nyumbani na anapata uchangamfu huko. Katika hali hizo ni sawa akaenda msikitini. Vinginevyo nyumbani ndio bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokana na misikiti ya Allaah. Hata hivyo nyumba zao ni bora kwao.”[1]

[1] Ahmad (2/76) na Abu Daawuud (567). Imesahihishwa na Ibn Khuzaymah (1684) na al-Haakim (755).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22783/هل-صلاة-المراة-ببيتها-افضل-حتى-في-الحرم
  • Imechapishwa: 22/08/2023