364 – ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Baada ya kumaliza kwetu kuswali – nafikiri alisema ´Aswr – Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitusimulia na kusema: “Sijui nikuelezeni au ninyamaze.” Tukasema: “Ikiwa ni kheri, ee Mtume wa Allaah, basi tueleze, na ikiwa siyo hivo, basi Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.” Akasema:

ما مِن مسلمٍ يَتطَهَّرُ، فيُتِمُّ الطهارةَ التي كتَبَ اللهُ عليه، فيصلّي هذه الصلواتِ الخمسَ؛ إلاَّ كانت كفاراتٍ لما بينها

“Hakuna muislamu yeyote anyejitwahirisha na akakamilisha ile twahara ambayo Allaah amemuwajibishia, na baada ya hapo akaswali hizi swalah tano, isipokuwa inakuwa ni kifutio cha madhambi yaliyo baina yazo.”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Naapa kwa Allaah! Nitakuelezeni maneno, lau kama isingelikuwa Aayah ndani ya Kitabu cha Allaah, basi nisingekuelezeni. Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

لا يتوضّأ رجلٌ فيحسنُ وضُوءَه، ثم يصلّي الصلاةَ؛ إلا غُفِرَ له ما بينهما وبين الصلاة التي تَليها

“Hakuna mtu anayetawadha na akafanya vizuri wudhuu´ wake kisha akaswali, isipokuwa husamehewa yaliyo baina yake na swalah inayofuata.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Imekuja vilevile kwa Muslim:

مَن توضّأَ للصلاةِ فأسبغَ الوُضوء، ثم مشى إلى الصلاةِ المكتوبةِ، فصلاّها مع الناس أو مع الجماعةِ أو في المسجدِ؛ غُفِر له ذنوبُهُ

“Yule mwenye kutawadha kwa ajili ya kuswali, akaeneza vizuri wudhuu´ wake, kisha akatembea kwenda katika swalah ya faradhi na akaiswali na watu, na mkusanyiko au msikitini, basi husamehewa madhambi yake.”

Imekuja katika upokezi wake mwingine tena:

ما مِن امرئٍ مسلمٍ تَحضُرُهُ صلاةٌ مكتوبةٌ فَيُحسِنُ وضوءَها وخشوعَها وركوعَها؛ إلا كانت كفارةَ لما قبلها من الذنوبِ، ما لم تُؤتَ كبيرةٌ  ، وذلك الدهرَ كلّه

“Hakuna muislamu yeyote ambaye atakutana na swalah ya faradhi ambapo akafanya vizuri wudhuu´ wake, unyenyekevu wake na Rukuu´ yake, isipokuwa itakuwa ni kifutio cha madhambi yaliyokuwa kabla yake, muda wa kuwa hajafanya madhambi makubwa. Hayo yanafanya kazi maisha mazima.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/268-269)
  • Imechapishwa: 22/08/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy