27. Shukurani ya kweli ni subira

Muhammad bin Kinaasah alimwandikia ndugu yake akimpa pole baada ya kufa mtoto wake:

“Allaah (Ta´ala) amekutunuku zawadi na akakulazimisha kumruzuku na kumwangalia sambamba na hilo ukachelea juu yake kupewa mtihani, ambapo ukawa na furaha kubwa. Baadaye Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akachukua zawadi Yake na akakutosheleza kutokana na kumwangalia na kupewa mtihani kwake, ambapo huzuni yako ikawa kubwa. Naapa kwa Allaah kama ungelikuwa ni mwenye kumcha Allaah, basi ungelifarijika kwa yale uliyopongezeka kwayo, na ungelipongezeka kwa yale uliyofarijika kwayo. Itakapokufikia barua yangu hii, basi isubirishe nafsi yako juu ya adhabu ambayo huwezi kuisubiri, na isubirishe nafsi yako juu ya thawabu ambazo huwezi kuzikosa. Vovyote msiba utavyokuwa mkubwa, basi kamwe haipotei furaha juu ya thawabu zake inayolingana na msiba wako. Hiyo ni huzuni ya kudumu.”

Baadhi wamesema:

Ukipatwa na msiba, basi subiri juu yake –

ni balaa kubwa kwa mtu kutosubiri kwa msiba wake

Mwingine akasema:

Unalipwa thawabu kwa aliyepotea –

kwa hivyo usimkose aliyeondoka na thawabu

Muhammad bin as-Sammaak alimwandikia Haaruun Rashiyd akimpa pole juu ya mtoto wake aliyekufa:

“Ukiweza kumshukuru Allaah (´Azza wa Jall) juu ya kifo chake kama ulivyomshukuru wakati alipokutunuku naye wakati alipozaliwa, basi fanya hivo. Wakati alipomchukua kutoka kwako sambamba na hilo alikuwekea akiba ya zawadi yako. Endapo atabaki basi hutosalimika kutokana na mtihani wake. Fikiria kukata kwako tamaa juu ya kifo chake na huzuni yako juu ya kufarikiana naye. Unaridhia maisha ya dunia juu ya nafsi yako na hivyo ukayaridhia juu ya mwanao? Kuhusu yeye amesalimika kutokana na uchafu ilihali wewe umebaki unaishi ndani ya khatari. Amani!”

Ibn-us-Sammaak alimpa rambirambi bwana mmoja akasema:

“Miongoni mwa utimilifu wa shukurani juu ya uzima ni kusubiri juu ya misiba. Anayetangulia hufanikiwa, na anayechelewa hukosa.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 109-111
  • Imechapishwa: 23/08/2023