Imepokelewa kwamba ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema baada ya mmoja katika wanawe kuaga dunia:

Maisha si vyengine isipokuwa namna hii, hivyo subiri –

janga linaloipata mali au kutengana na kipenzi

Mtu mwenye uzoefu wa maisha haogopi

mabadiliko yake ya nyakati zake mbili kwa ajili ya mwenye busara

Muhammad bin al-Husayn bin ´Ayyaash amesema: ´Abdullaah bin Wadhdhwaah amenihadithia:

“Alisimama ´Abdul-Malik karibu na kaburi la mwanawe akasema:

Maisha na masiku si vyengine isipokuwa kama unavoona –

janga linaloipata mali au kutengana na kipenzi

Mtu mwenye uzoefu wa maisha haogopi

mabadiliko yake ya nyakati zake mbili kwa ajili ya mwenye busara

Abu Bakr bin Abiyd-Dunyaa amesema katika “Kitaab-ul-´Azaa’”: al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia kuwa bwana mmoja katika Quraysh amesema juu ya mwanawe:

Nikikupoteza wewe, ee mwanangu kipenzi, katika maisha yangu

Sintokupoteza huko Aakhirah

Ulikuwa ni kilele changu, anayeondosha hamu yangu,

matangamano yangu na anayewepesisha moyo wangu

Abu Ya´quub al-Khuraymiy akimsifu mwanawe namna hii katika shairi:

Lau isingelikuwa kutaraji malipo juu yako –

tanzia ya aliyefikwa na msiba ni kubwa

Wewe ni ukurubisho wenye kunufaisha mbele ya Allaah

na fungu letu siku ya Qiyaamah ni kubwa –

ingelidhoofika huzuni yangu, ee mwanangu kipenzi

na wale wanawake wanaolia walikuwa wamesimama kwa miguu yao

Baadhi wamesema:

Kuna faida gani ya kuomboleza wakati mtu anapoondoka?

Je, kilichopotea kitarudi kwa kunung´unika?

Yote yanahusiana na kukubali, kujisalimisha na kusubiri

kile ambacho Mungu ameshakadiria

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 23/08/2023