Matendo mema yanayofanywa Makkah

Swali: Je, kuna utofauti inapokuja katika ubora wa swawm ya Makkah na mahali kwengine?

Jibu: Ndio, kila tendo jema Makkah lina ubora wake. Hili linahusu matendo yote mema. Isipokuwa swalah ambayo huzidishwa mara laki moja. Ama matendo mengine yana ubora na sifa ya kipekee. Hata hivyo hakuna kikomo maalum. Hata Madiynah pia inayo fungu katika hayo. Kwa mujibu wa dalili ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) matendo yanayofanywa Makkah huzidishwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha kuwa swalah moja ya Makkah inalipwa mara laki moja. Katika msikiti wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) swalah moja inalipwa mara elfu moja ukilinganisha na misikiti mingine. Kuhusu matendo mengine yanayo ubora ingawa hakukuwekwa ukomo wa kitu. Thawabu zinalipwa zaidi kukiwemo swawm, swadaqah, Tasbiyh, Tahliyl, usomaji wa Qur-aan, Twawaaf na mengineyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22782/هل-للصيام-في-مكة-فضل-عن-غيرها
  • Imechapishwa: 22/08/2023