Swali: Kuna muislamu aliyekuwa anajadiliana na mnaswara ambapo yule mnaswara akamtukana Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), yule muislamu na yeye akamtukana ´Iysaa (´alayhis-Salaam) ili kumkasirisha yule mnaswara bila ya kujua kuwa kitendo hichi ni kufuru. Je, anapewa udhuru kwa ujinga na ana nini juu yake?

Jibu: Ikiwa ni mjinga anatakiwa kubainishiwa ya kwamba lau angelikuwa ni mwenye kukusudia kweli na mwenye kufanyia kusudi angelikufuru. Lakini ujinga unamzuia na kufuru mpaka abainishiwe. Haijuzu kuwatukana Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (37) http://alfawzan.af.org.sa/node/2148
  • Imechapishwa: 13/07/2020