Swali: Kuna muislamu aliyekuwa anajadiliana na mnaswara ambapo yule mnaswara akamtukana Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), yule muislamu na yeye akamtukana ´Iysaa (´alayhis-Salaam) ili kumkasirisha yule mnaswara bila ya kujua kuwa kitendo hichi ni kufuru. Je, anapewa udhuru kwa ujinga na ana nini juu yake?
Jibu: Ikiwa ni mjinga anatakiwa kubainishiwa ya kwamba lau angelikuwa ni mwenye kukusudia kweli na mwenye kufanyia kusudi angelikufuru. Lakini ujinga unamzuia na kufuru mpaka abainishiwe. Haijuzu kuwatukana Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (37) http://alfawzan.af.org.sa/node/2148
- Imechapishwa: 13/07/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket