Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kila mtu ni mwenye kuifanyia matendo nafsi yake; kuna mwenye kujiuza na kujiachia huru na mwenye kujiangamiza.”
Kujiangamiza maana yake ni kujiuza. Kafiri hufanya matendo ambayo yana kumpelekea katika maangamivu. Hilo linakuwa kwa kafiri kuanza siku yake kwa kumuasi Allaah. Hata akianza siku yake kwa kula na kunywa, kula kwake na kunywa kwake ataadhibiwa kwayo siku ya Qiyaamah. Atahesabiwa kwayo. Kila kijipunje kidogo ambacho kafiri anatia mdomoni mwake ataadhibiwa kwacho. Kila kinywaji anachoweka katika mdomo wake, ataadhibiwa kwacho. Kila vazi analovaa, ataadhibiwa kwalo. Dalili ya hili ni maneno Yake (Ta´ala):
قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا
“Sema: “Nani aliyeharamisha mapambo ya Allaah ambayo amewatolea waja Wake navizuri katika riziki?” Sema: “Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia.” (07:32)
Haya ni kwa wale walioamini. Sio haki ya wengine:
خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ
“… kwa waumini pekee siku ya Qiyaamah.”
Bi maana hawatopata lolote siku ya Qiyaamah. Kinachopata kufahamika katika Aayah hii tukufu:
قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ
“Sema: “Nani aliyeharamisha mapambo ya Allaah ambayo amewatolea waja Wake na vizuri katika riziki?” Sema: “Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia maalum [kwa waumini pekee] siku ya Qiyaamah.”
ni kwamba ni haramu kwa wale wasiokuwa waumini na ni khaswa kwao siku ya Qiyaamah na wataadhibiwa kwayo.
Vilevile Allaah amesema katika Suurah “al-Maaidah”:
لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا
“Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mazuri katika vile walivyokula [kabla ya kuharamishwa].” (05:93)
Kinachopata kufahamika katika Aayah hii tukufu ni kwamba ni lawama kwa wale wasiokuwa waumini katika vile walivyokula.
Kafiri tokea pale anapoamka asubuhi ni mwenye kujiuza nafsi yake kwa yale yanayomwangamiza.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/193-194)
- Imechapishwa: 19/02/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)