Aina za watu katika furaha na madhara

Watu katika mlango huu – furaha na madhara – wamegawanyika sehemu mbili:

1 – Kila kile ambacho muumini amekadiriwa na Allaah kwake ni kheri. Akifikwa na madhara anakuwa ni mwenye subira juu ya makadirio ya Allaah, anasubiri faraja kutoka kwa Allaah na kutarajia thawabu kutoka kwa Allaah. Hilo linakuwa ni kheri kwake. Kwa hili anapata ujira wa wenye kusubiri.

Akipatwa na furaha, katika neema ya dini kama elimu, matendo mema, mali na watoto, anakuwa ni mwenye kumshukuru Allaah. Kushukuru kwake inakuwa kwa kumtii Allaah. Kwa sababu kushukuru hakukuwi kwa mtu kutamka tu kwa mdomo “Ninamshukuru Allaah.” Bali kushukuru inakuwa kwa kumtii Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo anamshukuru Allaah na hilo linakuwa ni kheri kwake. Hapo anapata neema mbili:

1 –  Neema ya dini.

2 – Neema ya dunia.

Neema ya dunia inakuwa kwa kule kufurahi. Neema ya dini inakuwa kwa kule kushukuru. Hii ndio hali ya muumini. Yeye katika hali zote anakuwa yumo katika kheri, sawa ikiwa atapatwa na furaha au madhara.

2 – Ama kafiri hali zake zote anakuwa katika shari. Akifikwa na madhara hawi ni mwenye subira. Bali inakuwa ni kama dunia nzima imemwangukia, anatukana wakati na zama, bali anafikia mpaka kumtukana Allaah (´Azza wa Jall).

Akifikwa na furaha hawi ni mwenye kumshukuru Allaah. Furaha hii inakuwa ni adhabu kwake Aakhirah. Kwa sababu kafiri hali anachokula na hanywi anachokunywa isipokuwa anapata madhambi kwa kitu hicho. Kitu hichohicho kwa upande mwingine sio madhambi kwa muumini. Lakini hata hivyo kwa kafiri inakuwa ni madhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/198-199)
  • Imechapishwa: 19/02/2023