Anaswali Sunnah wakati imamu anaswali faradhi

Swali: Anayemuona mtu mwenye kuswali Sunnah wakati ambapo imamu anaswali faradhi.

Jibu: Afunzwe na abainishiwe. Haijuzu. Afunzwe kwamba kitendo hicho hakifai. Baadhi ya wanazuoni, kama wanazuoni wa Ahnaaf, wanaona kufaa kuswali Raatibah. Ni kosa. Ni maoni dhaifu.

Swali: Sunnah ya Fajr?

Jibu: Si Sunnah ya Fajr wala nyingine.

Swali: Lakini mtu anapata dhambi?

Jibu: Anayejua anapata dhambi. Na asiyejua pengine akapewa udhuru kutokana na ujinga wake. Lakini anapata dhambi baada ya kujua.

Swali: Swalah yake ya Sunnah inaharibika?

Jibu: Ndio, inaharibika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22104/كيف-ينصح-من-يصلي-سنة-والامام-يصلي
  • Imechapishwa: 27/10/2022