Swali: Je, inafaa kumhukumu mtu kuingia Motoni ikiwa haswali na anafanya matendo ya makafiri?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwenyewe amemuhukumu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baina ya mtu na kufuru au shirki ni kuacha swalah.”

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”

Makafiri ni wenye kukatiwa Moto. Anayekufa juu ya ukafiri basi ni katika watu wa Motoni.

Swali: Mtu mmoja mmoja kwa dhati yake?

Jibu: Ni kwa kuenea. Ni mamoja kwa kuenea au mtu mmoja mmoja kwa dhati yake. Anayedhihirisha ukafiri anaambiwa kuwa ni kafiri. Abu Jahl ni kafiri na ni miongoni mwa watu wa Motoni. ´Utbah bin Rabiy´ah na Abu Twaalib wote ni miongoni mwa watu wa Motoni. Umethibiti ukafiri wao na wakafa juu ya ukafiri.

Swali: Lakini imetangaa katika vitabu vya ´Aqiydah ya kwamba mtu yeye kama yeye kwa dhati yake asishuhudiliwe Pepo wala Moto. Lakini tunataraji mema kwa wema na tunachelea kwa mtenda madhambi.

Jibu: Hapa ni pale ambapo bado yuko hai. Anapokufa juu ya ukafiri basi tunamshuhudia ukafiri na Moto. Waumini kwa ujumla wao tunawashuhudia kuingia Peponi na makafiri kwa ujumla wao tunawashuhudia kuingia Motoni. Ambaye itatambulika kuwa amekufa juu ya ukafiri basi ni miongoni mwa watu wa Motoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22105/هل-يحكم-بالنار-لمن-لا-يصلي
  • Imechapishwa: 27/10/2022