Anasafiri nje ya Riyaadh na kurudi siku hiyohiyo

Swali: Kuna bwana mmoja anafanya kazi nje ya mji wa Riyaadh na kila siku anasafiri umbali wa 80 km. Yeye na marafiki zake wengine wanaswali huko kazini Dhuhr na ´Aswr kwa mkusanyiko.

Jibu: Wanazingatiwa ni wasafiri katika huo mji wanakokwenda.

Swali: Lakini wanarudi Riyaadh kabla ya swalah ya ´Aswr.

Jibu: Ndio, hapana neno. Haina neno kwa msafiri akikusanya swalah kisha akarudi katika mji wake kabla ya wakati wa swalah ya pili. Vivyo hivyo hapana vibaya akikusanya katika wakati wa Maghrib kisha akafika katika mji wake kabla ya swalah ya ´Ishaa.

Swali: Lakini 80 km ndio huzingatiwa kiwango cha chini kabisa?

Jibu: Ndio.

Swali: Inafaa kwa msafiri kufupisha endapo atasafiri na kurudi siku hiyohiyo?

Jibu: Ndio, ikiwa safari yake ina umbali usiopungua 80 km.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22381/هل-يعد-مسافرا-من-يقطع-يوميا-ثمانين-كيلو
  • Imechapishwa: 11/03/2023