Swali: Je, dhahabu nyeupe inatolewa zakaah?

Jibu: Sijui dhahabu nyeupe.

Swali: Inauzwa sokoni na inaitwa dhahabu nyeupe?

Jibu: Thamani yake ikifika kile kiwango ambacho ni cha lazima kutoa zakaah inatolewa. Vivyo hivyo fedha. Haizingatiwi kuwa ni dhahabu hata kama watu wataiita hivo. Dhahabu haiwi isipokuwa nyekundu. Ikiwa thamani yake ni ya dhahabu na fedha itatolewa zakaah. Hapo ni pale ambapo thamani yake itafikia kile kiwango cha lazima.

Swali: Almasi?

Jibu: Almasi pia na kila kitu ambacho thamani yake itafikisha kile kiwango cha lazima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22377/ما-حكم-الزكاة-في-الذهب-الابيض-والالماس
  • Imechapishwa: 11/03/2023