Swali:  Mwenye kusahau Witr.

Jibu: Aiswali katika wakati wa Dhuhaa´ kabla ya Dhuhr. Aswali kile kitachomuwepesikia kabla ya Dhuhr. Mtume (Swallla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapokosa nyuradi yake ya usiku basi anailipa mchana. Hivo ndivo alivosema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Aiswali kwa njia ya shufwa na si witiri. Bi maana aiswali Rak´ah mbili mbili… Lililo karibu zaidi na usawa – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba [iwe wakati wa] Dhuhaa´ au Dhuhr. Kuhusu ´Aswr hapana. Amesema katika Hadiyth nyingine:

“Mwenye kukosa sehemu yake ya usiku ambapo akailipa mchana kabla ya Dhuhr ni kana kwamba ameilipa usiku.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22375/كيف-ومتى-يقضي-الوتر-من-نسيه
  • Imechapishwa: 11/03/2023