Picha za kwenye karatasi hazina neno?

Swali: Je, sanamu zinazokuwa kwenye karatasi zinaingia katika picha?

Jibu: Picha inaweza kuwa kwenye karatasi, kwenye vitambaa, kwenye ukuta, kwenye jiwe au kitu kinachojitegemea chenyewe.

Swali: Je, Malaika hawaingii nyumba ambayo ina picha ilioko kwenye mto au kitanda kinachotwezwa?

Jibu: Hapana, picha aina hiyo haizuii Malaika kuingia ikiwa inadharauliwa. Ikiwa kwenye mto au zulia haizuii Malaika kuingia.

Swali: Vipi kuswalia kwenye zulia hiyo?

Jibu: Hapana neno. Ikiwa inafaa kuitandaza basi inafaa pia kuswali juu yake. Lakini bora zaidi ni kuswali juu ya kitu kisichokuwa na michoro na hakishawishi. Bora ni kuswali kwenye kitu kisichokuwa na michoro na mapambo ili kisimshawishi mwenye kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22386/حكم-التصاوير-على-الورق-والوساىد-ونحوها
  • Imechapishwa: 11/03/2023