Anadaiwa Ramadhaan nne kwa sababu ya mimba na kunyonyesha

Swali: Mke wangu anadaiwa Ramadhaan tatu au nne anazotakiwa kulipa na hakuweza kuzifunga kwa sababu ya ujauzito au kunyonyesha. Hivi sasa ananyonyesha. Anauliza kama anapata ruhusa ya kulisha chakula kwa sababu anapata uzito mkubwa wa kulipa kwa idadi ya Ramadhaan tatu au nne?

Jibu: Hapana neno kwake kuchelewesha kulipa ikiwa ni kutokana na uzito anaopata kwa sababu ya ujauzito na kunyonyesha. Pale atakapoweza basi atatakiwa kuharakisha kulipa kwa sababu ana hukumu moja kama mgonjwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.” (02:185)

Halazimiki kulisha chakula.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/222) nr. (6608)
  • Imechapishwa: 25/04/2022