Swali: Katika Ramadhaan mtu akikasirika juu ya kitu na katika hali ya hasira akapiga kelele au akatukana – je, kitendo hicho kinaharibu swawm yake?

Jibu: Jambo hilo haliharibu swawm yake. Lakini linapunguza thawabu zake. Ni lazima kwa muislamu ajidhibiti na auchunge ulimi wake kutokamana na matusi, maapizo, usengenyi, umbea na mengineyo ambayo Allaah ameyaharamisha katika swawm na hali nyenginezo. Ingawa katika hali ya swawm ni khatari zaidi na kuna makokotezo ya ziada juu ya kuihifadhi ili swawm yake iwe kamili. Aidha anatakiwa kujiepusha na yale yanayowaudhi watu na kuwa sababu ya fitina, chuki na mifarakano. Amesema (Swalla Allaahu ´álayhi wa sallam) amesema:

“Itapokuwa ni siku ya funga ya mmoja wenu, basi asizungumze maneno machafu wala asipige kelele. Mtu akimtukana au akamgombeza, basi aseme: “Mimi ni mtu nimefunga.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/333) nr. (7825)
  • Imechapishwa: 25/04/2022