Swawm ya anayetokwa na damu isiyokuwa hedhi

Swali: Katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan nilikuwa mjamzito na nikatokwa na damu ya kawaida (نزيف) tarehe 20 Ramadhaan na niliendelea na swawm na sikula wala sikunywa. Nilikula siku nne nilizokuwa nimelazwa hospitali. Baada ya Ramadhaan nililipa zile siku nilizokula. Nifunge mara nyingine na mtoto bado yuko tumboni?

Jibu: Swawm yako ambayo ulikuwa unatokwa na damu ya kawaida haiathiriki. Ni kama mwanamke anayetokwa na damu ya ugonjwa. Swawm yako ni sahihi. Siku nne ulizofungua hospitalini kisha baada ya Ramadhaan ukazilipa zinakutosha na wala huhitajii kuzifunga mara nyingine.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (13168)
  • Imechapishwa: 25/04/2022