an-Nawawiy asiigwe katika mambo yanayohusu sifa za Allaah

Swali: Kuna ndugu wanaosema kuwa Imaam an-Nawawiy ni Ash´ariy inapokuja katika majina na sifa za Allaah. Je, hili ni sahihi na ni ipi dalili? Je, ni sawa mtu kuwasema vibaya wanachuoni kwa sura kama hii? Wengine wanasema kuwa ana kitabu chenye kuitwa “Bustaan-ul-´Aarifiyn” ambapo amefuata madhehebu ya Suufiyyah humo. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Ana makosa katika sifa za Allaah. Amefuata madhehebu ya wenye kupindisha maana sifa za Allaah na akakosea katika hilo. Hivyo asiigwe katika hilo. Lililo la wajibu ni kushikamana na imani ya Ahl-us-Sunnah ambapo wanathibitisha majina na sifa za Allaah zilizothibiti katika Qur-aan na Hadiyth Swahiyh kwa njia inayolingana na Allaah (Jalla wa ´Alaa); bila ya kupotosha, kukanusha, kuziwekea namna wala kuzilinganisha kwa mujibu wa maneno Yake (Subhaanah):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)

Kuna Aayah nyinginezo zenye maana kama hiyo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/164)
  • Imechapishwa: 23/08/2020