Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kufa juu ya Tawhiyd ya Ashaa´irah kabla ya kufikiwa na Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat, hakusikia kwa yeyote na hakuisikia. Lakini hata hivyo amekubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Ilaahiyyah. Hakuna aliyemzindua na kumkataza. Je, mtu huyu anapa udhuru au hapana?

Jibu: Jambo lake liko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ashaa´irah sio makafiri. Lakini wamekosea katika kuzipindisha maana baadhi ya sifa za Allaah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/162)
  • Imechapishwa: 23/08/2020