Amemwacha mke wa nne na anataka kuoa mke mwengine

Swali: Mwanaume akioa wanawake wanne kisha baadaye akamwacha mmoja katika wao. Je, mwanaume huyo yuko na kipindi cha kusubiri?

Jibu: Hapana, asubiri mpaka imalizike eda ya mwanamke huyo. Kwa sababu kipindi hicho mwanamke huyo bado ni mke wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 02/09/2023