Miongoni mwa wanazuoni walio msitari wa mbele ambao wana muda mrefu katika ulingano, ni muheshimiwa Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad, muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy, muheshimiwa Shaykh Swaalih as-Suhaymiy na muheshimiwa Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy.

Wanaume hawa wana bidii na kumtakasia nia Allaah katika ulinganizi. Wanawaraddi wale wanaotaka kupinda kutokana na ulingano kutoka katika njia yake sahihi, ni mamoja wamefanya hivo kwa kukusudia au pasi na kukusudia. Wanaume hawa wana mazoezi na uzoefu. Wanathibitisha maoni mbalimbali na wanaona tofauti kati ya kilicho sahihi na kisichokuwa sahihi.

Kwa hivyo inatakiwa kueneza kaseti na darsa zao na watu wanufaike nazo, kwa sababu ndani yake kuna faida kubwa kwa waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=1kaKejfv6Iw
  • Imechapishwa: 02/09/2023