02. Vipi ukoo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) upande wa mama yake?

Swali 2: Vipi ukoo wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) upande wa mama yake?

Jibu: Mama yake anaitwa Aaminah, msichana wa Wahb, mwana wa ´Abdu Manaaf, mwana wa Zuhrah, mwana wa Kilaab, mwana wa Murrah.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizaliwa ndani ya ndoa na hakuzaliwa nje ya ndoa. Allaah aliwakinga kutokana na hilo baba na mama zake wote.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 91
  • Imechapishwa: 02/09/2023