04. Anayofaa mwanamke kuonyesha mbele ya baba yake, kwa mtazamo wa al-Mawduudiy

Nilibainisha sehemu kidogo katika maelezo yangu kwa al-Mawduudiy aliyoyaweka mwishoni mwa kitabu chake ”al-Hijaab”. Humo nimetaja kuwa Hadiyth ya Qataadah kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi na Hadiyth ya Jurayj kuna wapokezi wanaokosekana katika cheni ya wapokezi, kwa sababu kuna pengo kubwa baina yake yeye na ´Aaishah. al-Mawduudiy amelikubali hilo, lakini hata hivyo ameona kuwa cheni zote mbili hizo zinaitia nguvu Hadiyth hiyo. Hoja yake ni eti moja wapo inaafikiana kabisa na nyingine. Lakini amepitwa (na sitaki kusema kuwa amelifumbia macho) na kwamba katika cheni inayokosa wasimulizi yanakosa yale yaliyopo katika cheni inayokosa Swahabah, nayo ni yale tuliyotaja kwenda kinyume na Qur-aan. Kitu pekee zinaafikiana ni lile tamko linalonasibishwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jambo linalokubainishia tofauti kati ya viwiili hivyo ni kwamba al-Mawduudiy anazijengea hoja kuthibitisha kuwa mwanamke hatakiwi kuonyesha chochote mbele ya wanamme, hata mbele ya baba na kaka, zaidi ya uso na mikono. Hicho ndicho kilichonifanya kukiwekea kitabu chake maelezo na wachapa vitabu wakamtaka kueneza maelezo yangu pamoja na kitabu. Humo nimetaja kuwa Hadiyth inayokosa Swahabah imetajwa kwa jumla na kwamba inaweza kufanywa maalum kwa dalili maalum na inayotambulika. Nimetaja baadhi yake katika maelezo yangu niliyoyaashiria. Ama kuhusu Hadiyth ambayo haina wasimuliaji, inayo kitu cha nyongeza. Kwani nyongeza inasema waziwazi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichukizwa na kitendo cha ´Aaishah kutoka mbele ya mpwa wake hali ya kuwa amejipamba, kitu ambacho kinapingana na Qur-aan. Nyongeza hiyo haipo katika ile Hadiyth ambayo inakosa Swahabah. Kwa maana nyingine Hadiyth hizo mbili ni zenye kutofautiana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 03/09/2023