Amejiharamishia mwanamke baadaye akataka kumuoa

566 – Nilimuuliza Shaykh wetu kuhusu mtu aliyemwambia mwanamke wa kando: “Wewe kwangu ni kama mama yangu” kisha baadaye akataka kumuoa. Je, anapaswa kutoa kafara ya kumfananisha mke na mama?

Jibu: Ikiwa atamuoa, basi anatakiwa kutoa kafara ya kiapo kwa sababu mwanamke huyo hakuwa mke wake. Hilo ni kutokana na maneno Yake (´Azza wa Jall):

لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ

”Kwa wale walioapa kujitenga na wake zao [kutokujamiiana]… ” (02:226)

Lakini hakuna chochote kinachompasa kufanya ikiwa hatomuoa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 194
  • Imechapishwa: 12/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´