Ambaye hakusimama tena Tahajjud anaandikiwa kuwa ameswali usiku mzima?

Swali: Mwenye kuswali pamoja na imamu wake katika swalah ya Tarawiyh na asisimame naye katika Tahajjud mwishoni mwa usiku – je, anazingatiwa kuwa amesimama usiku mzima?

Jibu: Mwenye kusimama na imamu wake mpaka akaondoka, basi anaandikiwa kuwa amesimama usiku mzima. Ikiwa imamu wao amewaswalisha mwanzoni mwa usiku mpaka mwisho, basi anapata thawabu za kusimama usiku mzima. Akiswali tena pamoja na wengine wanaoswali tena mwishoni mwa usiku, basi inakuwa ziada na haina neno. Lakini asiswali Witr mbili. Akiswali Witr na imamu wa kwanza asiswali Witr na imamu wa pili. Aswali kile kitachomsahilikia lakini asiswali Witr tena mara ya pili. Aswali pamoja naye na afanye shufwa kwa kuongeza Rak´ah moja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.”

Kwa mfano akiswali Witr katika msikiti Mtakatifu au kwenginepo pamoja na imamu aliyeswalisha mara ya kwanza, kama ameswali Witr na yule imamu wa kwanza basi asiswali Witr tena na imamu wa pili. Aswali na imamu huyu wa pili kile kitachomuwepesikia na asiswali Witr pamoja naye. Akiswali naye Witr ile Rak´ah moja ya mwisho, basi ataleta shufwa kwa Rak´ah nyingine moja. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11721/من-اكتفى-بالتراويح-مع-الامام-هل-يكتب-له-قيام-ليلة
  • Imechapishwa: 08/04/2023