Du´aa maalum kila baada ya Rak´a mbili za Tarawiyh

Swali: Baadhi ya watu kila baada ya Rak´ah mbili za swalah ya Tarawiyh wanaomba kwa kusema:

نسأل الله الهدى والرضا والعفو عما مضى

“Tunamuomba Allaah uongofu, ridhaa na msamaha wa yaliyotangulia.”

Jibu: Haina msingi. Du´aa hii haina msingi. Hata hivyo hapana neno kwa ambaye ataomba kile ambacho Allaah amemuwepesishia. Hakuna du´aa maalum kati ya Tasliym mbili. Lakini ni sawa kwa ambaye ataomba. Kuhusu kitu maalum hakuna du´aa iliyotajwa wala nyingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12915/حكم-تخصيص-دعاء-معين-بين-ركعات-التراويح
  • Imechapishwa: 08/04/2023