Rawaatib na Witr vinaswaliwa lini wakati wa kukusanya swalah?

Swali: Tuliswali Maghrib na ´Ishaa kwa kukusanya msikitini kwa sababu ya mvua na baridi. Ni lini tutaswali Rawaatib tutapokusanya swalah? Idadi yake inakuwa ngapi? Shufwa na Witr vinaswaliwa papohapo au ni lazima kuchelewesha?

Jibu: Unaposwali ´Ishaa na Maghrib katika wakati wa Maghrib, basi utaswali Sunnah ya Maghrib na Sunnah ya ´Ishaa baada ya hapo. Baada ya hapo ndio utaswali Witr hata kama ni baada ya Maghrib. Wakati wa Witr na Sunnah ya ´Ishaa umeingia kwa kutangulizwa ´Ishaa hata kama imekusanywa na Maghrib katika wakati wa Maghrib.

Vivyo hivyo Dhuhr na ´Aswr zinapokusanywa hali ya kuwa ni mkazi kwa sababu ya mvua au maradhi… hakuna Sunnah baada ya swalah ya ´Aswr. Huo ni wakati ambao imekatazwa kuswali. Dhuhr inapokusanywa na ´Aswr, basi hapo inadondoka Raatibah ya Dhuhr inayokuwa baada yake. Bora ni kuiwekea juu yake ´Aswr kabla ya kuswali Raatibah. Katika hali ya kukusanya kwa sababu ya mvua, maradhi na kadhalika inadondoka Raatibah inayoswaliwa baada ya Dhuhr. Lakini Raatibah ya kabla ya Dhuhr, ambayo ni Rak´ah nne, itaswaliwa kama kawaida. Baada ya Dhuhr kutaswaliwa ´Aswr kwa kuunganisha pasi na kizuizi na pasi na kupambanua na Raatibah ya Dhuhr inayoswaliwa baada yake.

Kuhusu Maghrib na ´Ishaa zinaswaliwa wakati usiokuwa wa makatazo. Ukishaswali ´Ishaa, basi utaswali Sunnah ya Maghrib, ambayo ni Rak´ah mbili, na utaswali baada yake Sunnah ya ´Ishaa, ambayo ni Rak´ah mbili. Ukitaka kuswali Witr utafanya hivo au pia unaweza kuiakhirisha katikati ya usiku au mwishoni mwa usiku. Jambo ni lenye wasaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12966/متى-تصلى-الرواتب-والوتر-عند-الجمع-بين-الصلاتين
  • Imechapishwa: 08/04/2023