Amenuia kuamka usiku kuswali lakini akadharurika

Swali: Mwanamme au mwanamke akitia nia ya kusimama usiku kuswali na asiweze anaandikiwa thawabu ya kile alichonuia?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja anapogonjweka au akasafiri, basi Allaah humwandikia yale aliyokuwa akiyafanya hali ya kuwa mzima na mkazi.”

Vivyo hivyo akipitiwa na usingizi, hakuzembea, anaandikiwa thawabu kama amesimama usiku. Lakini anatakiwa kuswali mchana kile kilichompita. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapokosa nyuradi zake za usiku kutokana na usingizi au maradhi, basi anaswali mchana kwa kukabili yale ambayo alitakiwa kuyafanya usiku. Hii ndio Sunnah. Ugonjwa au usingizi ukimshughulisha kutokana na kuswali Witr usiku na sehemu yake ya kisomo cha usiku, basi anayafanya mchana kabla ya Dhuhr. Hivi ndio bora. Thawabu zake zinakuwa kamili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11296/حكم-من-نوى-قيام-الليل-ثم-عجز-عن-ذلك
  • Imechapishwa: 08/04/2023