Aliyekuja amechelewa pale imamu anasujudu sujuud ya kusahau baada ya salamu

Swali: Ni kipi kinachomlazimu ambaye amekosa baadhi ya Rak´ah wakati imamu anaposujudu sujuud ya kusahau baada ya salamu? Je, atoe salamu pamoja na imamu kisha asujudu?

Jibu: Hapana. Atoe salamu akimaliza kukidhi kile kinachomlazimu. Ambaye amepitwa na baadhi ya Rak´ah atasujudu sujuud ya kusahau baada ya kulipa kile kilichompita. Akitoa salamu pamoja na imamu kwa kusahau, akasahau yeye mwenyewe au akasahau katika zile Rak´ah alizoswali mwenyewe, kusujudu kwake kunakuwa baada ya kumaliza swalah yake kabla ya kutoa Tasliym mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22263/حكم-المسبوق-لو-سجد-الامام-للسهو-بعد-السلام
  • Imechapishwa: 27/01/2023