Swali: Imethibiti kwa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) kumuona Allaah usingizini?

Jibu: Shaykh Taqiyy-ud-Diyn Ibn Taymiyyah ametaja kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaweza kuona nuru au maneno. Allaah hafanani na viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala).

Swali: Vipi kuhusu Muusa na ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam)?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Hatujafikiwa na kitu.

Swali: Kumuona Allaah inahesabika ni kitu maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana. Hata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuona. Alipoulizwa alisema:

”Niliona nuru. Ni vipi nitamuona?”

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Tambueni kuwa hakuna yeyote katika nyinyi atamuona Mola wake mpaka afe.”

Kumuona Allaah kunakuwa Aakhirah. Waumini watamuona siku ya Qiyaamah na watamuona Peponi. Kuhusu duniani hapana.

Swali: Vipi kuhusu kumuona usingizini?

Jibu: Kuhusu kumuona usingizini kunaweza kutokea.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22261/هل-تثبت-روية-الله-تعالى-في-المنام-للانبياء
  • Imechapishwa: 27/01/2023