Kuanza kutoa salamu ni lazima au inapendeza?

Swali: Kuanza kutoa salamu ni lazima au inapendeza?

Jibu: Allaah ndiye anajua zaidi. Hata hivyo udhahiri wa Hadiyth ni kwamba inapaswa kwa muumini asifanye uchoyo. Aharakishe kutoa salamu. Hii ndio Sunnah kwa muumini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Haki ya muislamu juu ya muislamu mwenzie ni sita; ukikutana naye mtoe salamu.”

al-Baraa´ amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamtuamrisha mambo saba” ambapo akataja moja wapo kueneza salamu.”

Kwa hivyo inatakikana kwa mtu kuiharakisha. Ni mamoja tuseme kuwa inapendeza kufanya hivo au ni lazima. Kuhusu kujibu ni lazima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ttps://binbaz.org.sa/fatwas/22274/هل-البدء-بالسلام-للوجوب-ام-للاستحباب
  • Imechapishwa: 27/01/2023