Swali: Ni yepi makusudio ya kuunga kizazi katika Hadiyth mbalimbali?
Jibu: Kuunga kizazi maana yake ni wale ndugu na jamaa. Ndugu wote ni kizazi chako. Walio karibu zaidi ni baba, mama, watoto na wajukuu.
Swali: Vipi ikiwa mtu anataka kuunga kizazi chake lakini wapo katika nchi nyingine?
Jibu: Anapaswa kuwaunga hata kama wako nchi nyingine. Awaunge kwa kuwaandikia, kuwatumia zawadi na kuwasaidia.
Swali: Kwa hivyo inatosha kuwatumia?
Jibu: Posta zipo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22281/ما-المراد-بصلة-الرحم-في-الاحاديث
- Imechapishwa: 27/01/2023