Sutrah ya maamuma baada ya imamu kutoa salamu

Swali: Je, baada ya Tasliym ya imamu Sutra ya imamu inabaki kuwa ni Sutrah ya maamuma aliyechelewa baadhi ya Rak´ah?

Jibu: Hapana. Ikiwa ni wepesi kwake kuweka Sutrah ni vyema. Vinginevyo akamilishe swalah yake hata kama ni pasi na Sutrah. Kukiwepo na Sutrah karibu yake ni vizuri akaiweka mbele yake ikiwa anakhofia asipite mtu mbele yake. Kwa sababu yuko katika msikiti Mtakatifu wa Makkah mbele ya Ka´bah hahitaji Sutrah. Hili linamuhusu mwanamme na mwanamke wote wawili.

Swali: Hili ni kuhusu msikiti Mtakatifu wa Makkah peke yake?

Jibu: Ndio. Kukiwa kuna msongamano na hawezi kuweka Sutrah basi ni mwenye kusamehewa. Ni mamoja yuko Madiynah au kwenginepo:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Swali: Kwa hivyo ni mahali popote?

Jibu: Mahali popote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22272/هل-سترة-الامام-بعد-تسليمه-سترة-للماموم
  • Imechapishwa: 27/01/2023