Alcohol katika matibabu, mafuta na manukato

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia alcohol au pombe kwa ujumla nikiwa na maana ya kuitumia katika kuchora samani, matibabu, mafuta, kusafisha, manukato na kuifanya siki?

Jibu: Kinacholevya kingi ni pombe. Ni mamoja kingi na kidogo chake. Ni mamoja inaitwa alcohol au majina mengine. Ni lazima kuimwaga na ni haramu kuihifadhi kwa ajili ya kuitumia na kunufaika nayo katika kusafisha, kama mafuta, kama manukato, kuigeuza siki au aina nyingine katika kunufaika nayo. Kuhusu kile kisicholewesha kingi chake sio pombe na inafaa kuitumia katika kujitia manukato, matibabu, kujisafisha majeraha na kadhalika.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzzaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (22/107) nr. (8684)
  • Imechapishwa: 02/06/2022